MOURINHO KUONGEZA WATATU CHELSEA

Wednesday, 10 June 2015

Mourinho wants three new signings - but is determined to keep Hazard


Meneja Wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwamba usajili wake wa kwanza anaoupa kipaumbele ni kuwalinda wachezaji bora waliopo wasiondoke klabuni hapo, lakini ameahidi kuongeza watatu katika kikosi kilichotwaa ubingwa msimu uliokwisha.

Baada ya Chelsea "The Blues" kufanikiwa kushinda taji la ligi msimu wa 2014-2015, mreno huyo ana nia ya kudumisha mawazo ya kushinda bila kufanya mabadiliko ya kutosha katika kikosi chake kilichotwaa taji hilo.

Ingawa kocha huyo anatafuta mchezaji wa kuziba nafasi ya mshambuliaji Didier Drogba ikiwa pamoja na kuongeza wachezaji wachache ili kuongeza ushindani wa ziada katika safu yake, Mourinho anatarajia kupambana na vilabu pinzani vitakavyojaribu kununua nyota wake.

"Misimu mingine, nilikuwa na furaha sana kuuza baadhi ya wachezaji, hata waliokuwa wazuri-lakini mwaka huu sina raha kuuza wachezaji wangu bora, kwa hiyo changamoto niliyonayo ni kuwafanya wabaki hapa," mreno huyo alinukuliwa na Mirror.

"Nikiwabakiza [Eden] HAzard, [Nemanja] Matic, [Branislav] Ivanovic, [Diego] Costa na [Cesc] Fabregas, hilo ni lengo kuu la kwanza."

"Nadhani tunahitaji wachezaji watatu-mshambuliaji, kwa sababu tumempoteza shujaa wetu [Drogba], beki na kiungo ili kuongeza ushindani zaidi, kuongeza damu mpya katika kikosi inaleta ushindani kwa wachezaji waliopo."

"Wanahitaji kutambua kuwa kuna mtu anasubiri nafasi zao-wao ni mabingwa sasa, ninahitaji hilo kudumisha namna ya ufanyaji wangu kazi. Lakini kimsingi, ninahitaji kuweka wachezaji wale wale, kikosi kile kile, meneja yule yule, na kuleta utulivu katika klabu."

0 comments:

Post a Comment