N'ZONZI KUTIMKIA KLABU ZA LONDON NA MAJOGOO WA JIJI LA LIVERPOOL;REMY SOKONI,JUVE YANASA,TOWNSEND ATIMKIA VILLA PARK,MATTIA PERIN NDANI SPURS

Friday, 19 June 2015

Stock City wakiwa na hamu kubwa ya kumuongezea mkataba mchezaji wao Steven N'zonzi timu za Arsenal,Liverpool na Tottenham zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.


Klabu za Juventus ya Italia na Athletico Madrid ya Hispania tayari zimefikia makubaliano ya ada ya uhamisho wa mshambuliaji Mario Mandzukic aliyejiunga na klabu hiyo ya Hispania akitokea  klabu ya Bayern Munich.Usajili huo utaigharimu klabu ya Juventus kiasi cha €18 milion kwa mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Italia.

Klabu ya Chelsea imemuweka sokoni mshambuliaji wake Loic Remy huku wakiweka kiwango cha pauni 15 milioni kama ada ya uhamisho wake kwa timu zitakazo muhitaji.

Andros Townsend wa klabu ya Tottenham anataka kubaki klabuni hapo kwa msimu ujao licha ya klabu ya Aston Villa kuhitaji huduma yake.

Klabu hiyo ya London pia ipo mbioni kumsajili golikipa wa timu ya Genoa Mattia Perin kutokana na golikipa wao Hugo Lloris kutakiwa na klabu kadhaa huko Ulaya.

0 comments:

Post a Comment