
Changamoto kubwa aliyokuwa akipambana nayo Msuva ni kurejea kwa winga Mrisho Ngassa kwenye kikosi cha Yanga akitokea Simba lakini kijana huyo aliweza kupambana nayo na kufanikiwa kulinda nafasi yake ya kucheza kikosi cha kwanza chini ya makocha Ernie Brandts, Marcio Maximo ambaye mara nyingi alikuwa akimtumia kama mchezaji wa akiba na sasa Mholanzi Hans van der Pluijm.
Bado ana mapenzi na muziki
Pamoja na kufanikwa katika soka lakini Msuva bado hajasahau zile staili za muziki alizokuwa akifufundishwa kule THT, mara kadhaa amekuwa akiwafundisha wachezaji wenzake pindi wanapo shangilia bao na alifanya hivyo hata kwa Mbrazili Geilson Santana Santos JAJA, alipofunga bao la pili katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 huku Msuva akifunga moja.
Msuva amekuwa rafiki wa karibu na Ngassa katika ushangiliaji kutokana na wachezaji wote hao kuonekana kuvutiwa sana na muziki hasa ule wa Msanii anayetamba kwa sasa Naseb Abduli ‘Diamond’ na staili yake ya Ngololo.
Kufunga mechi tatu mfululizo
Kitu kingine ambacho hukijui kutoka kwa Msuva ndiye mchezaji aliyeweze kufunga katika mechi tatu mfululizo katika msimu uliomalizika na yeye kuwa mfungaji bora mechi ambazo alifunga mfululizo ni ile kati ya Yanga na Kagera Sugar iliyofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam ambapo walishinda mabao 2-1 yeye akifunga bao la kwanza na Amissi Tambwe akifunga la pili.
Mechi ya pili ilifanyika ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga dhidi ya Mgambo JKT iliyotoka kuwafunga wapinzani wao Simba na wao kushinda kwa mabao 2-0 yeye akifunga bao la kwanza dakika ya 77 na katika dakika ya 83 Amissi Tambwe akifunga bao la pili na kuipa Yanga uongozi wa ligi.
Mechi ya tatu ilifanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam dhidi ya JKT Ruvu Msuva akafunga tena mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 na kumfanya afikishe mabao 11 na kumpiku mshambuliaji wa Azam Didier Kavumbagu.
Aliipa Yanga matumaini kombe la Shirikisho
Pia Msuva ndiye mchezaji aliyesababisha Yanga kupata bao moja katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Etoile du Sahel, baada ya kuangushwa kwenye eneo la penalty na kipa wa timu hiyo na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufunga penati hiyo japo hadi dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1
Mafanikio hayo ya msimu uliopita ni ishara njema ya kuendelea kufanya vizuri kwa Msuva kutlingana na umri wake pamoja na wachezaji aliokuwa nao kwenye kikosi cha Yanga ambao mara zote wamekuwa wakimchezesha.








0 comments:
Post a Comment