PETR CECH NDANI, OSPINA NJE ARSENAL, "NI HERI KUCHEZA ASTON VILLA KULIKO CHELSEA"-BEGOVIC

Friday, 26 June 2015

ARSENAL-CECH, OSPINA, SZCZESNY:


Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.


Petr Cech atafanyiwa vipimo vya afya siku ya Leo kabla ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na klabu hiyo. Licha ya kubakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, klabu ya Chelsea itapokea dau la pauni milioni 15 kwa ajili ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 33.


CHELSEA-BEGOVIC:


Kipa anayewindwa kwa hali na mali na klabu ya Chelsea Begovic amesema ni heri ajiunge na klabu ya Aston Villa ambayo imeonesha nia ya kuhitaji huduma yake kuliko akawe kipa namba mbili kwa miamba hao wa Uingereza klabu ya Chelsea. Baada ya Petr Cech kutimka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Arsenal, Chelsea wanatafuta msaidizi wa Thibaut Courtois.

0 comments:

Post a Comment