BAADA YA KUMFANYIA UCHAFU CAVANI, KLABU YAKE YAMTUPIA VIRAGO JARA, PETR CECH KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA LEO...

Friday, 26 June 2015

FC MAINZ-GONZALO JARA:

Embedded image permalink

Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.

"Anatambua kuwa ofa yoyote ikija, anaweza kuondoka," mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Christian Heidel aliiambia Bild. "Hatuwezi kuvumilia hilo. Zaidi ya kumuwekea kidole, hata hivyo, kilichofuatia baadae ndicho kilinipatia hasira. Nachukia maigizo zaidi ya kitu chochote."

ARSENAL-PETR CECH, TOTTENHAM-YEVHEN KONOPLYANKA:



Taarifa kutoka Eurosport zinasema kwamba golikipa anayetarajia kujiunga na klabu ya Arsenal kutoka klabu ya Chelsea Petr Cech atafanyiwa vipimo vya afya leo hii. Huku taarifa hizo zikienea kwa kasi pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Tottenham wanamngojea winga wa Dnipro Yevhen Konoplyanka ambaye leo yupo njiani akielekea Spurs kufanyiwa vipimo vya afya.

JUVENTUS-OSCAR:



MChezaji wa klabu ya Chelsea OScar amesema kuwa hawezi kujiunga na klabu ya Juventus inayoonesha nia kubwa ya kumhitaji mchezaji huyo raia wa Brazil.
"Ni vigumu kabisa na hakuna ukweli wowote katika hilo. Oscar hatoondoka Chelsea."

0 comments:

Post a Comment