ROBIN VAN PERSIE KUTIMKIA ZAKE UTURUKI...

Thursday, 18 June 2015



Kocha wa Galatasaray Hamza Hamzaoglu ametanabaisha kuwa klabu yake ina nia ya kumleta Uturuki mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie.

Muelekeo wa mchezaji huyo klabuni hapo haujafahamika, huku kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal akifikiria kumuondoa mholanzi mwenzake katika klabu hiyo ili kuacha nafasi kwa mshambuliaji mpya.

Mabingwa wa Italia Juventus na klabu ya Serie A Lazio zote zimehusishwa katika mbio za kumuwania mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal, ambaye alifunga magoli 10 kati ya mechi 27 za Ligi Kuu msimu uliopita.

Galatasaray inaonekana kuwa mbele katika mbio hizo, na Hamzaoglu-ambaye aliiongoza klabu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Uturuki msimu wa 2014-2015-kuwa na nia ya kumleta mshambuliaji huyo katika kikosi chake.

"Tunataka kusajili wachezaji ambao wataimarisha kikosi chetu na pia watawafurahisha mashabiki," aliiambia Fanatik.

"Hakuna meneja anayeweza kusema 'Hapana' kwa Van Persie. Hata hivyo hatuwezi kutumia kuzidi kiwango chetu. Tuna matumaini sisi na yeye tutafikia muafaka."

0 comments:

Post a Comment