
Chelsea inamnyemelea kiungo wa Zenit St Petersburg Axel Witsel ambapo kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho amepanga kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.
The Blues imemuelezea Witsel kuonesha kumuhitaji huku klabu hiyo ikionesha nia ya kutaka kujiimarisha katika kiungo, wakati John Obi Mikel akipanga kutimka klabuni hapo kujiunga na klabu za Uturuki au Mashariki ya Kati.
Witsel, mwenye umri wa miaka 26, anampango wa kutimka katika klabu yake ya sasa Zenit St Petersburg msimu huu na ana nia ya kujiunga na miamba wa Italia klabu ya Juventus, lakini chelsea wanaamini mchezaji huyo atajiunga na klabu yao.

Witsel anaaminika kuwa atakuwa mbadala wa kudumu wa Mikel Obi ambaye anaweza kutimka klabuni hapo baadaya ya kuambia yupo huru kuondoka.
Chelsea wanaimani kubwa ya kumchukua mchezaji huyo kwakuwa anatumia wakala mmoja na kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho.
Zenit walitumia dau la euro milioni 40 kupata saini ya kiungo huyo kutoka klabu ya Benfica mwaka 2012 lakini amesema anataka kujiunga na klabu nyingine baada ya kunyakua taji na mabingwa hao.
Kwa sasa, Chelsea wanafikiria kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Augsburg Baba Rahman. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 20 amehusishwa na kujiunga na klabu ya Chelsea baada ya kufanya vema Bundesliga.
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
AXEL WITSEL NA BABA RAHMAN NDANI, MIKEL OBI NJE CHELSEA...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment