RONALDINHO KUTUPIWA VIRAGO MEXICO

Wednesday, 10 June 2015

Kocha mkuu wa timu ya Queretaro ya nchini Mexico imebainisha mipango yake ya kuachana na mwanasoka nguli wa Brazil Ronaldinho Gaucho kwa kushindwa kucheza katika kiwango chake cha juu kama ilivyokua awali.



Kushuka kwa kiwango cha mwanandinga huyo kimechagiwa na umri wake kuwa mkubwa. Mchezaji huyo kwa sasa ana umri wa miaka 34 hivyo kushindwa kufikia makali yake tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Mexico.

"Inategemea na sababu mbalimbali, lakini swala ni kwamba yeye [Ronadinho] hatoshiriki tena kwa ajili yetu," Vucetich aliwaambia waandishi wa habari Jumanne.

Akiendelea kubainisha hayo kocha huyo ametanabaisha kuwa nje ya uwanja kimasoko, mchezaji huyo amekua sehemu kubwa ya mafanikio ya klabu hiyo lakini kwa sasa timu yake inataka wachezaji wenye nguvu ya kuisaidia timu katika nyanja zote, nje na ndani ya uwanja.

Ronaldinho amefunga mabao nane kunako klabuni hapo tangu alipowasili akitokea Athletico Mineiro ya Brazil mwaka 2014.

 

0 comments:

Post a Comment