
Kiungo mkongwe na mahiri wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, Andrea Pirlo anatarajia kukutana na maofisa wa klabu ya soka ya Sidney, huku mwakilishi wa klabu hiyo akijaribu kumshawishi kutua nchini Australia na kuachana na mpango wa kujiunga na New York City inayoshiriki ligi ya soka nchini Marekani.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 hivi sasa, amepata kuiwakilisha timu yake ya taifa mara 113.
Pirlo ambaye alishindwa kuisaidia timu yake kutamba mbele ya Barcelona katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa Ulaya jumamosi iliyopita wakichapwa mabao 3-1, anahusishwa na kuihama klabu yake ya Juventus baada ya kubakiwa na msimu mmoja tu katika mkataba wake.
Pamoja na kuenea kwa taarifa za kiungo huyo kuhamia klabu anayoichezea kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard, New York City ya nchini Marekani, lakini mmoja wa mawakala wa klabu ya Sidney ya nchini Australia amekaririwa akisema wanamhitaji mchezaji huyo kwa udi na uvumba.
“Kazi yangu ni moja tu hapa nchini Italia. Kama Pirlo ataondoka hapa Turin, basi nitamshawishi ajiunge na timu yetu ya Sidney” alisema afisa huyo na mwakalishi wa klabu hiyo.
Wakala huyo aitwaye Lou Sticca amethibitisha kuwa Sidney inahitaji wachezaji wakubwa ili wazibe mapengo yaliyoachwa wazi na wachezaji kadhaa nyota walioihama klabu hiyo.
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
TIMU YAMSHAWISHI KIUNGO ANDREA PIRLO AJIUNGE NAYO...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment