RONALDO AVUNJA REKODI YA PELE NA DE LIMA...

Tuesday, 16 June 2015



Siku hizi michuano imeongezeka sana tofauti na miaka ya zamani na hiyo ni moja ya sababu zinazowapa nafasi wachezaji wa generation hii kuwa na nafasi ya kuvunja rekodi nyingi za wachezaji wa zamani.

Cristiano Ronaldo baada ya kufunga hat trick kwenye Portugal Vs Armenia imempeleka juu ya wakongwe wa Brazil Pele na De Lima.

Rekodi hiyo inahusu magoli ambayo wamefunga kwenye timu za taifa ukitoa magoli ya mechi za kirafiki.

Kwenye magoli ya mechi za mashindano Ronaldo De Lima ana magoli 41, Pele ana magoli 43 na Cristiano ametimiza magoli 44. Magoli yote hata yamefungwa wakiwa kwenye mechi za mashindano.

cris

0 comments:

Post a Comment