
Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama ‘Simba watatu’ kiko katika maandalizi yake ya mwisho kuikabili timu ya taifa ya Slovenia katika mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya Euro 2016, huku mshambuliaji nyota na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney akikaribia kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa timu hiyo.
Katika mchezo huo utakao fanyika siku ya jumapili, Uingereza wanaongoza kundi wakiwa na pointi 15 katika michezo 5 waliyocheza kwa maana ya kushinda michezo yao yote ya awali, hawana majeruhi na wanatarajia kushinda katika mchezo huo kujiongezea nafasi ya kufuzu mapema iwezekanavyo.
Lakini kuelekea mchezo huo, mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ‘Wazza’ ndio stori kubwa kutokana na ukweli kwamba amebakiza magoli mawili tu, kuifikia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo inayoshikiliwa na mkongwe Bob Chalton.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hivi sasa, ameifungia Uingereza magoli 47 hadi sasa, huku Bob Chalton akiwa amefunga magoli 49.
Rooney na Bob Chalton wamejikuta katika hali hiyo hata katika ngazi ya klabu ambapo pia Chalton ndiye mfungaji bora wa klabu ya Manchester United huku Wayne Rooney ‘Shreak’ akiikaribia kwa ukaribu rekodi hiyo.
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa Rooney kuzivunja rekodi hizo zote mbili kutokana na ukweli kwamba bado ana miaka kadhaa mbele ya kufanya vizuri katika klabu na taifa.
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
ROONEY KUVUNJA REKODI YA BOB CHALTON JUMAPILI
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment