SAMI KHEDIRA ATIMKIA JUVENTUS...

Tuesday, 9 June 2015




Juventus imethibitisha kuwa itamsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira baada ya mkataba wake na klabu hiyo kuisha baadae mwezi huu.

Msimu uliopita mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani alikataa kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea klabu hiyo msimu ujao.

Khedira amekuwa akihusishwa na kurejea tena Bundesliga kujiunga na Schalke 04 huku timu za Uingereza kama Chelsea na Arsenal zikionesha nia ya kumtaka kiungo huyo lakini mshindi huyo wa kombe la dunia amechagua kuelekea mjini Turin.

"Klabu ya Juventus imepata saini ya Sami Khedira leo," taarifa iliyotolewa rasmi na tovuti ya Bianconeri siku ya Jumanne.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 atajiunga na miamba hao wa Italia kutoka Real Madrid kama mchezaji huru tarehe 1/7/2015. Sami Khedira amekubaliana na miamba hao mkataba utakao muweka klabuni hapo mpaka tarehe 30/6/2019.

Bianconeri bosi, Massimiliano Allegri ana mpango wakuongeza wachezaji wenye viwango vya juu na wenye uzoefu wa kimataifa katika klabu hiyo.

Khedira atahitaji kupambana ili kuweza kupata namba katika kikosi cha kwanza mbele ya viungo wengine kama Claudio Marchisio, Arturo Vidal, Andrea Pirlo na Paul Pogba.


0 comments:

Post a Comment