SANCHEZ KUMLETA ARTURO ARSENAL, SCHNEIDERLIN KUSAINI MIAKA 4 MAN UTD, MADRID WAKATAA DAU LA MAN UTD, POGBA KUTUA MAN CITY KABLA YA STERLING...

Friday, 26 June 2015

ARSENAL-ARTURO VIDAL:



Klabu ya Arsenal inajiandaa kutoa dau la pauni milioni 21 kumpata kiungo wa Juventus Arturo Vidal. Mchezaji huyo wa Chile ana nia ya kuungana na mchezaji mwenzake wa taifa Alexis Sanchez ambaye alitua klabuni hapo msimu uliopita akitokea Barcelona..

MANCHESTER UTD- SERGIO RAMOS:



Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa  dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.



Manchester United wapo mbioni kukamilisha usajili wa kiungo Morgan Schneiderlin wiki ijayo. Mfaransa huyo anataraji kusaini mkataba wa miaka minne klabuni hapo.



Manchester United imepanga kukataa ofa itakayotolewa na klabu ya Ujerumani Bayern Munich kwa ajili ya kumsajili winga Angel Di Maria. Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola anatamani kumsajili winga huyo huku mashetani hao wakiwa hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina.

REAL MADRID-NICOLAS OTAMENDI:



Real Madrid wanajiandaa kuhamia kwa Nicolas Otamendi kama mbadala wa beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos anayehusishwa na kutimka klabuni hapo kuelekea Manchester United.

MAN CITY-PAUL POGBA:



Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.

0 comments:

Post a Comment