
Nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati Brazili ikicheza dhidi ya Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazili kufungwa kwa goli 1-0.
Nahodha huyo wa Brazil alioneshwa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi kupulizwa kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Jumatano iliyopita. Neymar alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi mchezaji Pablo Armero wa Colombia mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo huo.

Awali alifungiwa kucheza mechi moja, lakini baadae shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South America Football Confederation) liliongeza kifungo na faini ya dola 10,000 za Kimarekani baada ya Neymar kugundulika kuwa alimtolea maneno machafu mwamuzi Enrique Osses raia wa Chile. Kwahiyo sasa adhabu ya Neymar ni kifungo cha kutocheza mechi nne pamoja na faini ya dola 10,000 za kimarekani.
Naye Carlos Bacca wa Colombia amefungiwa kucheza mechi mbili na faini ya dola 5,000 za kimarekani baada ya kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye mchezo huo ambapo yeye alimsukuma Neymar mara baada ya kumpiga Armero kwa mpira.

Lakini shirikisho hilo la mpira la America ya Kusini limesema, rufaa ikowazi wa wote waliopewa adhabu na Brazil wanaweza kupinga maamuzi hayo yaliyotolewa kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya Venezuela utakaopigwa leo (Jumamosi) usiku kuamkia kesho (Jumapili).
Kwasasa Brazil wanaoongoza kundi C na wanakutana na Venezuela ambao wametoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Peru lakini wakiwa wameshinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Colombia.
Awali Neymar alianza kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana kwenye soka pale alipojaribu kufunga goli kwa kutumia mkono lakini baadae ‘akambabua’ na mpira Pablo Armero na kutaka kumpiga kichwa Jeison Murillo.
Kukosekana kwa Neymar kutamfanya kocha wa Brazil Carlos Dunga amtumie Robinho, Coutinho, au Douglas Costa kama mbadala wa Neymar kwenye mechi ijayo dhidi ya Venezuela.

Dunga amekuwa akiwatumia Robinho na Douglas Costa kwenye mazoezi ili kujaribu kutengeneza uwiano mzuri kati yao wakati pia kiungo wa Liverpool Philipe Coutinho anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwake tangu kuanza kwa mashindano.
Robinho amejumuishwa kwenye kikosi cha Dunga mwaka jana baada ya kuikosa michuano ya kombe la dunia wakati huo kocha akiwa Scolari. Robinho ambaye alishawahi kukipiga Real Madrid, Manchester City na AC Milan kwasasa anacheza kwenye klabu ya Santos ya Brazil.
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
UJEURI WAMPONZA NEYMAR, AFUNGIWA MECHI NNE NA FAINI JUU...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment