SONG KUELEKEA CHELSEA,CARL JENKINSON AONGEZWA MKATABA ARSENAL,MAN UNITED YAIPIKU ARSENAL KWA DAYOT ,LIVERPOOL WAMSAKA FERNANDO LLORENTE & CARLOS BACCA........

Saturday, 20 June 2015

CHELSEA-ALEX SONG

Chelsea imeingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa klabu ya Barcelona Alex Song. West Ham wanajaribu kupata saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon kwa uhamisho huru, lakini Chelsea huenda ikatoa dau la £5m amabazo zinahitajika na klabu ya Barca kama Jose Mourinho anahitaji kuimalisha safu ya kiungo.


LIVERPOOL-FERNANDO LLORENTE & CARLOS BACCA
Liverpool 'plotting £36m raid for two of Europe's deadliest strikers'  Liverpool 'plotting £36m raid for two of Europe's deadliest strikers'
Baada ya kushindwa kufikia makubaliano na klabu ya Aston Villa ya £ 32,500,000 kama ada ya mchezaji Christian Benteke,Liverpool wanataka kumsajili mshambuliaji wa Juventus Fernando Llorente na mchazaji wa Sevilla Carlos Bacca.


MANCHESTER UNITED-DAYOT UPAMECANO

Manchester United wameipiku klabu ya Arsenal kwa kumsaini beki wa Valenciennes Dayot Upamecano mwenye umri wa miaka 16. Kijana huyo ataungana na wenzake katika kikosi cha United cha vijana.


ARSENAL-CARL JENKINSON

Arsenal wanatarajia kumpa mkataba mpya beki wa kulia Carl Jenkinson klaba ya kumpeleka mchezaji huyo kwa mkopo kwa awamu nyingine, baada ya beki huyo wa kulia kuichezea West Ham kwa msimu wa 2014-15.


0 comments:

Post a Comment