
Mwanasheria wa a Yanga Frank Chacha ameiambia Goal kuwa Kaseja si mchezaji wa Yanga kwasababu alijitoa mwenyewe kwa kuandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kwa madai kwamba hakulipwa pesa yake ya usajili.
Chacha amefafanua kuwa, wachezaji wa mpira ni waajiriwa kama waajiriwa wengine ndio maana Kaseja na Jaja wameshtakiwa kwenye mahakama ya kazi ya ndani na sio mhakama nyingine. Chacha aliendelea kusema kuwa, kwa kuwa Kaseja alikuwa ni mwajiriwa wa Yanga na ameamua kuacha kazi mwenyewe, kesi ya madai dhidi yake haimzuii yeye kuendelea kucheza mpira na kama anataka kusajiliwa kwenye timu nyingine yuko huru kufanya hivyo.
“Tunachokitaka Yanga ni madai yetu kwa kuvunja mkataba na tumezungumza naye na tupo tayari kutoa barua maalumu ya kumruhusu kuondoka na kusajiliwa na timu nyingine itakayo muhitaji,”amesema Chaha.
Klabu ya Stand United ilikuwa ikihitaji saini ya kipo huyo aliyewahi kutamba na klabu ya Simba kwa misimu 10 pamoja na timu ya taifa ya Tanzania kwa muda mrefu kwa ajili ya msimu ujao na pia kipa huyo anahusishwa kurudi timu yake ya zamani Simba ambayo ilishindwa kumuongezea mkataba misimu miwli iliyopita kwa madai ameshuka kiwango.








0 comments:
Post a Comment