NGASA AONEKANA MAZOEZINI YANGA...

Monday, 22 June 2015

Ngasa aonekana mazoezini Yanga
Mrisho Ngasa aliyejiunga na Free State Stars ya Afrika Kusini, kwa ajili ya kuichezea msimu ujao leo amefanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo kwenye uwanja wa Karume
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga Mrisho Ngasa aliyejiunga na Free State Stars ya Afrika Kusini, kwa ajili ya kuichezea msimu ujao leo amefanya mazoezi na kikosi cha timu hiyo kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumaliza mazoezi Ngassa akaiambia Goal, amerejea Yanga kufanya mazoezi kwa lengo la kujiweka fiti kabla ya kujiunga na timu yake mpya inayoshiriki ligi Kuu ya Afrika Kusini PSL.

“Nimeichagua Yanga kwa sababu hapa nikama nyumbani na sikuondoka kwa ubaya na katika maisha yangu ya soka naamini ipo siku nitarudi kuitumikia kwa mara nyingine,”amesema Ngassa.

Mashabiki wengi waliofurika kutazama mazoezi ya timu yao walilazimika kulisukuma gari la mchezaji huyo alipokuwa akiondoka baada ya mazoezi huku wengine wakisema wapo tayari kurudisha pesa za Free State ili kumrudisha winga huyo mwenye kasi ya pekee anapokuwa uwanjani.

Ngassa amejiunga na Free State ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka minne kucheza ligi ya PSL, kuanzia msimu ujao na timu hiyo inamatarajio makubwa kutoka kwake.

0 comments:

Post a Comment