ARSENAL YAONGEA NA WAKALA WA PEDRO,AC MILAN YARUDI KWA IBRAHIMOVIC,TOTTENHAM YAMSAKA YANNICK...

Monday, 6 July 2015

ARSENAL - PEDRO



Arsenal wamefanya mazungumzo na mwakilishi wa mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Pedro kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo msimu huu.

Chanzo: Independent
Jumatatu, Julai 6, 2015 00:29

AC MILAN - IBRAHIMOVIC



Licha ya kuwasajili Carlos Bacca na Luiz Adriano, Milan bado wanamatumaini ya kumnasa Ibrahimovic. Hata hivyo Rossoneri itamlazimu afanye jitihada za juu na kutoa ofa ya kutosha ili waweze kumnasa mchezaji huyo.

Chanzo: Corriere dello Sport
Jumatatu, Julai 6, 2015 07:40

MANCHESTER UNITED - FERNANDO MUSLERA



Manchester United imetenga kiasi cha euro milioni 35 kwa ajili ya golikipa wa Galatasaray Fernando Muslera. Golikipa huyo wa Uruguay amekuwa akitambuliwa kama mrithi wa David de Gea.

Chanzo: Vatan
Jumatatu, Julai 6, 2015 00:26

TOTTENHAM - YANNICK FERREIRA



Tottenham wameripotiwa kutenga kiasi cha £18 milioni kwa ajili Yannick Ferreira Carrasco. Timu hiyo ya Londoni ya kaskazini ilipeleka euro milioni 14 ambazo zilikataliwa na Monaco kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Chanzo: Daily Star
Jumatatu, Julai 6, 2015 00:31

ROMA - JUAN CUADRADO



Klabu ya Roma imerejea kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa winga wa Chelsea Juan Cuadrado.

Chanzo: Tuttosport
Jumatatu, Julai 6, 2015 07:16


PSG & MONACO - HACHIM MASTOUR



Paris Saint-Germain na Monaco zote zimeonesha nia ya kumsajili kiungo wa Ac Milan mwenye miaka 17 Hachim Mastour.

Chanzo: L'Equipe
Jumatatu, Julai 6, 2015 07:31


FIORENTINA, GATASARAY & NAPOLI - RAFFAEL



Fiorentina , Galatasaray na Napoli wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Manchester United Rafael. Mchezaji huyo wa kimataiffa wa Brazili anachukuliwa kama mchezaji wa akiba pale Old Trafford na anatazamiwa kuondoka  klabuni hapo, pia klabu mbili za Ligi Kuu zinamhitaji.

Chanzo: Daily Mail
Jumatatu, Julai 6, 2015 16:57


0 comments:

Post a Comment