LUIS NANI ATUA FENERBAHCE RASMI...

Monday, 6 July 2015

FENERBAHCE - LUIS NANI

Van Persie would succeed at Fenerbahce, says Nani

Klabu ya Fenerbahce imetangaza kumsajili Nani kutoka Manchester United.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa ureno aliwasili nchini Uturuki siku ya Jumapili kwa ajili ya vipimo vya afya ili kukamilisha dili la kumnyakua mchezaji huyo baada ya klabu ya Super Lig kukubaliana na  Red Devils.

Nani signs for Fenerbahce

Na klabu hiyo imethibitisha kuwa winga huyo mwenye miaka 28 atakuwa mchezaji rasmi wa Fenerbahce siku ya jumatatu saa 17:00 jioni katika uwanja wa Sukru Saracoglu, ambapo watawaalika mashabiki na waandishi wa habari kuhudhuria hafla hiyo.

Nani alizungumza kwa furaha huku akiwa na shauku ya kucheza katika jiji la Istanbul baada ya kupokelewa na mashsbiki wengi uwanja wa ndege.



"Kwa kweli ninafuraha kuwa hapa," alisema.

"Mimi naona hii ni kama fursa mpya katika kazi yangu. Pia ni fursa ya kujionesha mwenyewe. Pia nahitaji kuwa na mafanikio.

"Niliwaona mashabaki wakija kunitazama na nilikuwa na furaha sana. Nataka niwaoneshe mpira wangu wa ukweli.Daima huwa nafanya kile kilicho bora pale ninapoweza.

"Fenerbahce ni klabu niliyokuwa naifaham. Fenerbahce ni klabu yenye malengo ya kuwa klabu kubwa."



Nani, aliecheza Old Trafford kwa miaka nane,alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Sporting Lisbon msimu wa 2014-15, na kucheza mechi 27 za Primeira Liga.

0 comments:

Post a Comment