BAADA YA KUTUPIA GOLI 3 "HAT-TRICK", WENGER AMPATIA NAFASI KIKOSI CHA KWANZA...

Thursday, 16 July 2015

Arsenal won't loan out Akpom again, insists Wenger

Baada ya mshambuliaji chipukizi wa kilabu cha vijana cha Arsenal Chuba Akpom kutupia magoli matatu katika mchezo dhidi ya mastaa wa Singapore, kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema anataka kumuweka mshambuliaji huyo kwenye kikosi cha kwanza msimu huu na hatomtoa tena kwa mkopo.

Akpom amefanikiwa kutokea kwenye kikosi cha wakubwa mara nne tu tangu alipojiunga na timu ya watoto akiwa na miaka 6, lakini mwezi wa pili aliongeza mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo.

Amevichezea kwa mkopo vilabu kadhaa zikiwemo timu za Brentford, Coventry City and Nottingham Forest ndani ya miaka miwili iliyopita ambapo alishindwa kuonesha makali yake, lakini Arsene Wenger amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo kijana atapewa nafasi ya kung'aa kwenye kikosi cha kwanza hivi karibuni.

"Hapana, haendi tena kwa mkopo," Wenger aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo wa nusu fainali katika ziara yao huko Asia. "Nilimpeleka kwa mkopo msimu uliopita maana niliamini ndicho aichokuwa akihitaji.

"Lakini msimu huu hapana, ninampango wakumuweka pamoja nasi. Inategemea na utendaji kazi na tabia na ana samani ya kuwa kipaji kikubwa. Na, baada ya hapo, kuwa mchezaji mwenye uwezo wiki baada ya wiki, hayo ndio malengo.

"Sasa inategemea na yeye. Kiasi gani sifahamu. Inampatia moyo kufanya vema na kuongeza juhudi zaidi. Ni mchezaji kijana na itamuongezea kujiamini. Namna ambavyo wachezaji wengine wanavyoonesha kujiamini ndani ya chumba cha kubadili nguo ni muhimu pia.

"Inaweza kukusaidia. Lakini tusisahau kuwa ni mechezo ya kirafiki. Ana kipaji kizuri lakini anapaswa kufanya kazi na kuonesha hicho katika kila mchezo."

0 comments:

Post a Comment