CHRISTIAN BENTEKE KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA NDANI YA MASAA 48 YAJAYO...

Sunday, 19 July 2015



Baada ya klabu ya Liverpool kufikia makubaliano na klabu ya Aston Villa juu ya uhamisho wa mshambuliaji Christian Benteke, mchezaji huyo anategemea kufanyiwa vipimo vya afya.

Daktari wa kilabu hicho anatazamiwa kuelekea UK kutoka katika ziara ya timu hiyo huko Australia kukamilisha vipimo vya afya vya Benteke ndani ya masaa 48 yajayo.

Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 hatoungana na wechezaji wengine katika ziara hiyo.

Benteke alijiunga na Aston Villa akitokea Genk mwaka 2012 kwa ada ya pauni milioni 7, akifanikiwa kufunga magoli 49 katika michezo 101.

Baada ya kumuuza Raheem Sterling kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu klabu ya Manchester City kwa ada ya pauni milioni 49, Liverpool iliamua kumnyatia mshambuliaji huyo.

Benteke, ambaye amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na klabu ya Aston Villa, alifanikiwa kutupia magoli 12 katika michezo 12 msimu uliopita na kuisadia timu ya Tim Sherwood kutoshuka daraja.

Chanzo: Sport Football
Jumapili, 7/19/2015 09:57

0 comments:

Post a Comment