
Mashabiki wengi wa Arsenal hawafurahishwi na kitendo cha kocha wao Arsene Wenger kutulia kipindi hiki cha usajili wakati wanaamini kwamba Mfaransa huyo anatakiwa kutafuta mshambuliaji mmoja wa kati. "A central Striker".
Wakiwa wamemsaini Petr Cech ambaye tayari ameonesha ubora wake, mashabiki wa Arsenal wanajiamini kwamba Francis Coquelin na Santi Cazorla ni viungo wanaoweza kuwapa ubingwa.
Aaron Ramsey na Jack Wilshere pia ni viungo wa kati wanaotosha kuipa Arsenal mafanikio, lakini safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Olivier Giroud na Theo Walcott haiwezi kutimiza ndoto zao.
Kiukweli Giroud alipata wakati mgumu msimu wa 2014/2015 na sasa mashabiki wanasikia tetesi kuwa klabu yao inataka kumsajili Karim Benzema na Gonzalo Higuain, lakini Wenger amekanusha.
Siku za karibuni Higuain amechemsha sana na inamaanisha Wenger anatupia macho kwa Benzema ambaye bado anahitajika Real Madrid.
Giroud atafurahia kuondolewa katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal?
Mfaransa huyo amezungumzia hali hiyo hapa chini:
"Sifikirii swali hili kiukweli. Najaribu kuangalia zaidi maandalizi yangu ya msimu mpya. Tunafanya vizuri sana kama timu, kitu cha msingi siku zote kwangu ni kuona timu inaimarika, najitahidi siku zote kujitolea kadri niwezavyo. Kama atakuwepo straika mwingine, itakuwa vizuri kwa timu nzima kwasababu ushindani ni mzuri kwa kila mtu".
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
GIROUD AMKARIBISHA MSHAMBULIAJI MPYA ARSENAL...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment