HABARI ZA USAJILI MAJUU...

Tuesday, 14 July 2015

PSG-DI MARIA:



Usajili wa winga wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria ambae ndio chaguo la kwanza la kocha Laurent Blanc upo mbioni kukamilika kwa ada ya euro milioni 60.

Chanzo: Le Parisien
Jumanne, 7/14/2015 06:58

MAN CITY-BRUYNE:



Manchester City wameandaa dau la pauni milioni 35 ili kumnasa kiungo Kevin De Bruyne,japo wanapata ushindani toka kwa PSG na Bayern lakini bila shaka kiungo huyo atarejea Ligi ya Uingereza.

Chanzo: Daily Express
Jumanne, 7/14/2015 11:10

ROMA-DZEKO:



Klabu ya Manchester City imeiambia klabu ya Roma waongeze dau kufikia pauni 20 milioni ili kumpata mchezaji Edin Dzeko. Mratibu wa michezo wa kilabu hicho alipewa taarifa hizo alipokuwa Uingereza kwaajili ya kuzungumzia usajili wa mchezaji huyo.

Chanzo: talkSPORT
Jumanne, 7/14/2015 10:55

AJAX-SANOGO:



Mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo amekubali kujiunga na timu ya Ajax kwa mkopo wa muda mrefu.

Chanzo: De Telegraaf
Jumanne, 7/14/2015 00:25

MAN UTD-CAVANI:



Manchester United ipo kwenye mazungumzo na timu ya PSG juu ya kumnasa Edinson Cavan ila klabu hiyo ya Parc des Princes imeiomba Manchester United kumjumuisha Angel Dimaria kama sehemu ya malipo.

Chanzo: The Sun
Jumatatu, 7/13/2015 23:48

0 comments:

Post a Comment