DE GEA-MAN UTD:

Dili la mlinda mlango wa klabu ya Manchester Utd David de Gea kuuzwa katika kilabu cha Real Madrid limekufa japokuwa kilabu hicho kimemuuza kipa wake Iker Casillas. Kocha wa Manchester Utd Louis van Gaal hatomruhusu kipa huyo kutimka klabuni hapo msimu huu japokuwa amebakiza miezi 12 katika mkataba wake.
Hata hivyo mchezaji huyo amekasirishwa na kitendo cha Jorge Mendes juu ya hali ya uhamisho wake kuelekea Real Madrid na amepanga kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao.
Chanzo: Marca
Jumatano, 7/15/2015 08:05
SOUTHAMPTON-CLASIE:

Klabu ya Feyenoord inatazamia tena kuweka historia ya usajili wa klabu hiyo baada ya klabu ya Southampton kupanga kutoa kitita cha euro milioni 15 kumnyaka kiungo wa klabu hiyo Clasie.
Chanzo: De Telegraaf
Jumatano, 7/15/2015 07:48
MARSEILLE-FACUNDO RONCAGLIA:

Klabu ya Marseille yenye makazi yake Ufaransa inatazamiwa kumtafuta mbadala wa Rod Fanni na wamesema wapo kwenye mazungumzo na klabu ya Fiorentina kwa ajili ya usajili wa Facundo Roncaglia.
Chanzo: RMC
Jumatano, 7/15/2015 07:07
WEST HAM-RABIOT:

Ripoti zimeelezea kuwa mama yake Rabiot, ambaye ni wakala wa mchezaji huyo, yupo kwenye mazungumzo na klabu ya West Ham huku mchezaji huyo akipanga kutimka katika klabu yake ya sasa PSG.
Chanzo: Le Parisien
Jumatano, 7/15/2015 06:57
ROMA-MASCHERANO:

Ripoti kutoka klabu ya Roma zinaelezea kuwa klabu hiyo inamuwania mlinzi wa kati wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Javier Mascherano na imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo huku klabu hiyo ikiamini itamleta mchezaji huyo Stadio Olimpico.
Chanzo: Gazzetta dello Sport
Jumatano, 7/15/2015 06:47
WATFORD-LEX IMMERS:

Mchezaji wa klabu ya Feyenoord Lex Immers amesema amefurahishwa na klabu ya Watford kumuhitaji. Ripoti zinasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatamani kutua Ligi Kuu ya Uingereza.
Chanzo: Algemeen Dagblad
Jumatano, 7/15/2015 06:46
CHELSEA-PEDRO:

Klabu ya Chelsea ipo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 21.4 kumpata mchezaji wa Barcelona Pedro Rodriguez lakini mchezaji huyo amepanga kukutana na kocha wake Luis Enrique siku ya Jumatano (Leo) kuzungumzia maisha yake ya mbeleni katika klabu hiyo.
Chanzo: Irish Times
Jumanne, 7/14/2015 23:27
OTAMENDI-MAN UTD:

Mlinzi wa klabu ya Valencia Nicolas Otamendi amepanga kufanya mgomo kuishinikiza klabu yake kumuuza katika kilabu cha Manchester United.
Chanzo: The Sun
Jumanne, 7/14/2015 23:24
MAN UTD-ROMERO:

Manchester United wapo kwenye mazungumzo na mlinda mlango wa timu ya taifa ya Argentina Sergio Romero. Klabu ya Roma pia inavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Sampdoria mapema msimu huu.
Chanzo: Sky Sport Italia
Jumanne, 7/14/2015 23:23
ARSENAL-FAOUZI GHOULAM:

Klabu ya Arsenal imetoa ofa ya pauni milioni 7 kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Napoli Faouzi Ghoulam.
Chanzo: Daily Express
Jumanne, 7/14/2015 16:08
PSG-DI MARIA:

PSG wanafuraha kufikia makubaliano ya mshahara wa Angel Di Maria wa pauni 200,000 kwa wiki ambao unatazamiwa kumleta mchezaji huyo Parc des Princes.
Chanzo: Daily Mirror
Jumanne, 7/14/2015 15:28
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
TETESI ZA USAJILI ULAYA...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment