JUVENTUS INAMUWANIA OZIL, MAN UTD INAMTAKA MULLER OLD TRAFFORD, "RAMOS NA CASILLAS WAESHIMIWE"-MATEOS

Friday, 10 July 2015

JUVENTUS-MESUT OZIL:


Klabu ya Juventus amesema kuwa itamchukuwa kiungo wa klabu ya Arsenal endapo viungo wake wawili Paul Pogba na Arturo Vidal watatimka klabuni hapo msimu huu. Pogba anawindwa na klabu ya Manchester City pamoja na klabu ya Manchester City huku Arsenal wakionesha nia ya kumtaka Vidal.

REAL MADRID-CASILLAS, RAMOS, MARCELO:

Casillas & Ramos deserve better - Mateos

Beki wa Zamani wa klabu ya Real Madrid David Mateos amesema Ramos na Casillas wanahitaji heshima na ameisihi klabu hiyo pamoja na mashabiki kutosahau mambo mazuri ambayo wachezaji hao wameifanyia klabu hiyo. Casillas anategemea kujiunga na klabu ya Porto huku klabu ya Manchester United ikimuwania nahodha msaidizi wa klabu hiyo Sergio Ramos.


Habari nyingine kutoka Real Madrid ni kuwa mchezaji wa klabu hiyo raia wa Brazili Marcelo ameongeza mkataba utakaomuweka klabuni hapo kwa misimu mitano ijayo.

CRYSTAL PALACE-CABAYE:


Baada ya kushindwa kuonesha makali yake katika klabu ya PSG, mchezaji wa zamani wa Newcastle Cabaye amerejea rasmi Uingereza na amesaini mkataba na klabu ya Crystal Palace kwa ada ya pauni milioni 10 ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Newcastle Alan Pardew.

MANCHESTER UTD-THOMAS MULLER:


Huku mshambuliaji wa klabu ya Manchester Utd Robin van Persie akijandaa kutimka klabuni hapo kujiunga na klabu ya Fenerbahce, mashetani hao wekundu wapo tayari kushinikiza kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Thomas Muller kama mbadala wa Robin.

ZLATAN: NINGEPENDA KUCHEZEA BAYERN:


Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amedhihirisha kuwa angependa kukipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa kuwa anavutiwa sana na Bundesliga.  

0 comments:

Post a Comment