ARDA TURAN ATUA BARCELONA RASMI...

Friday, 10 July 2015

Arda signs five-year deal with Barcelona

Klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa mchezaji wa Atletico Madrid Arda Turan baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo siku ya Ijumaa.

Wiki iliyopita klabu ya Barcelona ilikubaliana na Atletico Madrid ada ya euro milioni 41 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki, japokuwa Barcelona wana haki ya kuukataa uhamisho huo kwa gharama ya euro milioni 4.1 kama mrithi wa Josep Maria Bartomeu ataingia madarakani kwa kuwa anadhani Arda hana nafasi katika kikosi hicho.

Hata hivyo, Arda Turan amesisitiza kuwa haogopi kurudishwa kwenye klabu yake ya Vicente Calderon (Atletico Madrid).

"Sina wasi wasi, mimi ni mcheza mpira," mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa. "Nipo hapa kuisaidia Barcelona ipate mafanikio zaidi. Vitu vingine sio vyangu kuhofia."

Arda pia aliutupilia mbali uvumi kuwa yeye ndiye mrithi wa Xavi aliyetimka klabuni mapema baada ya msimu 2014-2015 kuisha kujiunga na klabu ya Al Sadd.

"Kwanza kabisa, hakuna anayeweza kuwa mrithi wa Xavi kwa kuwa ni mchezaji bora," aliongezea winga huyo. "Alikuwa ni nyota na utambulisho wa Barcelona na Hispania."

"Mimi ni mchezaji tofauti. Mimi sio Xavi. Lakini nitajaribu kusaidia kwa uwezo wangu binafsi na staili yangu."

Embedded image permalink

0 comments:

Post a Comment