" KUPOTEZA FAINALI INAUMA....." ASEMA MESSI

Tuesday, 7 July 2015

Messi: There's nothing more painful than losing a final

"Hakuna kitu kinachoumiza zaidi kwenye mpira kama kupoteza mchezo wa fainali," Messi aliandika katika ukurasa wake wa Facebook.

"Lakini sihitaji kuyabeba machungu kwa kipindi kirefu napenda kusema ahsante kwa kila mtu ambaye ameonesha ushirikiano kwa kipindi hicho chote kigumu."



Taarifa zisizothibitishwa kutoka nchini Hispania zinadai kwamba Messi alipendekezwa kuwa mchezaji bora wa mechi lakini mchezaji huyo alikataa tuzo hiyo kufuatia kushindwa kwa Argentina kwenye mchezo huo.

Pia familia ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ilishambuliwa siku ya fainali mwishoni mwa wiki, wakati sehemu ya vyombo vya habari nchini Argentina vilikuwa mhimu kwa nyota huyo mzaliwa wa Rosario pamoja na wachezaji wenzake hata baada ya kupoteza fainali hiyo.

0 comments:

Post a Comment