MAN UTD YAMUWANIA NAVAS NA GAITAN, PEDRO ATAMANI KUJIUNGA PSG, R.MADRID IMEGONGA HODI KWA CASILLA...

Thursday, 9 July 2015

MANCHESTER UTD-KEYLOR NAVAS:



Manchester United inamtegemea mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid Keylor Navas kuwa sehemu ya makubaliano ya kumuuza David De Gea kwa klabu ya Real Madrid, ingawa usajili wowote hauna uhusiano na Sergio Ramos kwani mashetani wekundu wana mpango wa kumshusha  beki huyo wa kati klabuni hapo.

Chanzo: Marca
Alhamisi, 7/9/2015 12:41

REAL MADRID-NICOLAS OTAMENDI:



Real Madrid imekata tamaa ya kumpata mlinzi Nicolas Otamendi kwasababu wanaamini kuwa mlinzi huyo wa klabu ya Valencia amekubali kujiunga na klabu ya Manchester United.

Chanzo: Daily Mirror
Alhamisi, 7/9/2015 12:31

PSG-PEDRO RODRIGUEZ:



PSG wanategemea kumnasa mchezaji wa Barcelona Pedro Rodriguez. Mshambuliaji huyo anampango wa kutimka klabuni hapo kutafuta nafasi katika kikosi cha kwanza mahala pengine na atafurahi kama atajiunga na PSG.

Chanzo: Marca
Alhamisi, 7/9/2015 12:08

REAL MADRID-KIKO CASILLA:



Real Madrid wanategemea mpango wao wa kumpata mlinda mlango wa Manchester United David De Gea utaendelea vizuri mpaka siku za mwisho za dirisha la usajili. Miamba hiyo ya Hispania inajipanga kumsajili Kiko Casilla kutoka Espanyol kwa ajili ya kuwa na mlinda mlango katika michezo ya maandalizi ya msimu.

Chanzo: Daily Mirror
Alhamisi, 7/9/2015 11:50

MANCHESTER UTD- NICO GAITAN:



Manchester United wapo tayari kutoa pesa pamoja na wachezaji Rafael au Javier Hernandez baada ya kuanza mazungumzo ya kumnasa Nico Gaitan. Hata hivyo mashetani wekundu watamuhitaji mchezaji huyo wa Benfica endapo watamuuza Angel Di Maria.

Chanzo: A Bola
Alhamisi, 7/9/2015 11:10

0 comments:

Post a Comment