"MANCHESTER UNITED ITAMPATA DAMIAN," KOCHA WA TORINO ATHIBITISHA...

Thursday, 9 July 2015



Kocha wa Torino Giampiero Ventura amethibitisha kwamba dili la kumuuza mlinzi wao Matteo Damian kwa klabu ya Manchester United imekamilika.

Mtandao wa Goal unafahamu kuwa Manchester United imekubali kulipa dau la euro milioni 20 ili kumnasa beki wa kulia mwenye umri wa miaka 25 na inategemewa kutangazwa hivi karibuni.

"Ni kweli, Damian atacheza katika ligi ya Mabingwa akiwa na Manchester United," kocha huyo aliliambia jarida la Sky Sport la Italia.

"Matteo anastahili timu bora na siku zote amekuwa na ndoto ya kuchezea Ligi ya Mabingwa, sasa ni wakati wake.

"Ndani ya kipindi cha miaka minne tangu Damian amejiunga na Torino akitokea AC Milan, tumetoka Serie B na kuweka changamoto kubwa kwa timu zenye ubora wa juu na pia kuwa na muamko wakutaka kushiriki Ligi ya Europa.

"Tumefanya kazi na Damian kwa miaka mingi, nadhani ni wakati muafaka wakumpatia muda wa yeye kufanikisha ndoto zake za kushiriki Ligi ya Mabingwa."

Manchester United pia inamuwania mlinzi wa Argentina Nicolas Otamendi na bado wana matumaini ya kumnasa beki wa kati Sergio Ramos.

Chanzo: Goal.com
July 9,2015

0 comments:

Post a Comment