PEDRO AMEKUBALI KUTUA CHELSEA, BENTEKE KUTUA MAN UTD, ARSENAL IMEREJEA TENA KWA MANOLAS...

Sunday, 12 July 2015

CHELSEA-PEDRO:



Mchezaji wa klabu ya Barcelona Pedro Rodriguez amekubali kujiunga na klabu ya Chelsea baada ya kufanya mazungumzo ya simu na meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho na Cesc Fabregas alimshauri mshambuliaji huyo kutua Chelsea ambao walikuwa Mabingwa wa Ligi msimu uliopita.

Chanzo: Sport
Jumapili, 7/12/2015 08:13

MAN UTD-BENTEKE:



Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amefanya usajili wa mshambuliaji kuwa muhimu zaidi na amepanga kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke.

Chanzo: The Sun
Jumapili, 7/12/2015 07:15

EVERTON, ASTON VILLA, CRYSTAL PALACE-JORDAN AYEW:



Timu tatu kutoka Uingereza Everton, Aston Villa na Crystal Palace zinamuwania mshambuliaji wa klabu ya Lorient Jordan Ayew. Klabu ya Lille imehusishwa pia na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo lakini huenda wakashindwa kumsajili kutokana na bei yake kuwa kubwa kutokana na timu za Uingereza kumuwania.


Chanzo: L'Equipe
Jumapili, 7/12/2015 08:40

ROMA-DZEKO:



Roma imekubaliana na klabu ya Manchester City kuhusiana na usajili wa Edin Dzeko. Mshambuliaji huyo ataelekea Serie A kwa mkopo lakini Roma watakuwa na uchaguzi wa kumsajili kwa ada ya euro milioni 20 (£14.3m).

Chanzo: La Repubblica
Jumapili, 7/12/2015 08:36

MAN UTD-RAMOS AND NAVAS:



Klabu ya Manchester Utd imeiambia klabu ya Real Madrid kuwajumuisha wachezaji Sergio Ramos pamoja na Keylor Navas kwenye dili lao la kumsajili mlinda mlango David De Gea.

Chanzo: Marca
Jumapili, 7/12/2015 07:45

ARSENAL-MANOLAS:



Klabu ya Arsenal imeamsha tena matamanio yao ya kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Roma Kostas Manolas. Beki wa kati wa Manchester United Jonny Evans pia amehusishwa na kujiunga na washika bunduki hao wa Londoni.

Chanzo: Daily Star
Jumapili, 7/12/2015 07:45

MAN CITY-STERLING:



Manchester City wamewasilisha dau la tatu kwa klabu ya Liverpool lenye thamani ya pauni milioni 40 kwa ajili ya kumnasa winga wa klabu hiyo Raheem Sterling.

Chanzo: The Sun
Jumapili, 7/12/2015 07:13

0 comments:

Post a Comment