SABABU ZA PETR CECH KUCHAGUA JEZI NAMBA 33 AKIWA ARSENAL...

Sunday, 12 July 2015

Cech 3

Petr Cech ametangaza namba ya jezi  yake atakayokuwa akitinga akiwa langoni kuitumikia Arsenal.

Bila ya ubishi atakuwa mlinda mlango namba moja kuelekea msimu mpya wa ligi, hivyo basi Cech ameamua kuchagua namba 33 kama namba sahihi kwake akiwa klabuni hapo.

Cech ali-tweet kutoa sababu iliyomfanya achague kuvaa jezi yenye namba hiyo hiyo;





”Natumaini nitakuwa uti wa mgongo wa timu-mgongo una pingili 33...”

Huku baadaye pia akiongeza: “Naanza ukurasa mpya nikiwa na umri wa miaka 33 nikiwa nimecheza michezo 333 ya ligi kuu Uingereza…ni chaguo rahisi tu hilo”.

0 comments:

Post a Comment