PODOLSKI ATUA GALATASARAY RASMI...

Saturday, 4 July 2015

GALATASARAY - PODOLSKI



Klabu ya Galatasaray imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji huyo mwenye uzoefu katika kikosi cha taifa, aliichezea mechi chache timu yake ya Taifa katika Kombe la Dunia ambapo Ujerumani waliibuka mabingwa. Mchezaji huyo alishindwa kuonesha cheche akiwa na klabu ya Arsenal na kujikuta akikosa namba kwenye kikosi cha kwanza na kumpelekea kusukumwa kwa mkopo katika klabu ya Inter ambapo alifanikiwa kufunga goli moja kwenye mechi 19.

Lakini mchezaji huyo mwenye miaka 30 anaimani yupo vizuri pia anaamini yupo mahali ambapo atarejesha heshima yake kwa kupambana na klabu za Ulaya ambazo zinashiriki  Ligi ya Mabingwa na kutazamwa na mashabiki wengi.

"Mwaka uliopita Galatasaray walitoa ofa ya kunisajili," alisema Podolski. "Lakini mwaka huu kulikuwa na maslahi mazuri zaidi. Pia wazazi wangu walitaka nije hapa.

"Galatasaray walikuwa mabingwa mwaka jana.Tutapambana kuwa mabigwa katika miaka ijayo, sisi tunataka kupanda ngazi za juu zaidi.

"Nimekuwa nikiifuatilia Galatasaray kwa muda mrefu.Nafahamu kuna hali nzuri katika uwanja huo.

"Mashabiki wa Galatasaray wamenipa sapoti na wamefurahishwa na ujio wangu. Huu ni uamuzi mkubwa kwangu kwa kuamua jambo hili."


0 comments:

Post a Comment