VAN PERSIE KUONDOKA UNITED,CAZORLA ASAKWA NA ATLETICO,CHELSEA WAMNYATIA GERSON...

Saturday, 4 July 2015

MANCHESTER UNITED - VAN PERSIE, SCHNEIDERLIN & RAMOS



Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Fenerbahce baada ya kufikia makubaliano na klabu hiyo.

Chanzo: Guardian
Jumamosi, Julai 4, 2015 15:09



Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya pili kwa ajili ya Morgan Schneiderlin baada ya klabu ya Southampton kukataa ofa ya awali £20m.

Chanzo: Guardian
Jumamosi, Julai 4, 2015 10:22



Haijalishi ni kiasi gani cha pesa klabu ya Real Madrid watatoa kwa Sergio Ramos, Mhispania huyo ana nia ya kuondoka. Mchezaji huyo mwenye miaka 29 anahisi kuondoka Bernabeu na mwenyewe anahitaji kupata uzoefu katika ligi kuu na anahitaji kujiunga na Manchester United.

Chanzo: Marca
Jumamosi, Julai 4, 2015 00:14

CHELSEA - JUAN CUADRADO & GERSON



Klabu ya Chelsea imeamua kumbakiza Juan Cuadrado msimu huu japo mchezaji huyo hakuwa na mwanzo mzuri katika kipindi alichokuwa Stamford Bridge.

Chanzo: EL PaĆ­s
Jumamosi, Julai 4, 2015 13:57



Chelsea wameanza mazungumzo na klabu ya Fluminense juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa klabu hiyo Gerson. klabu ya Juventus tayari imeandaa ofa ya euro milioni 17(£12.1m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye miaka 18, wakati klabu za  Manchester United na Barcelona zimeonesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo pia.

Chanzo: Tuttosport
Jumamosi, Julai 4, 2015 07:47

PSG - KEVIN TRAPP & PATRICK ROBERTS



Kevin Trapp amefikia makubaliano binafsi na klabu ya PSG kwa ajili ya uhamisho wake msimu huu, hata hivyo mabigwa hao wa Ufaransa bado wanakibarua kigumu kwani wanahitaji kuishawishi klabu ya Eintracht Frankfurt kukubali mpango huo wa kumsajili mlinda mlango huyo.

Chanzo: Bild
Jumamosi, Julai 4, 2015 08:39



Paris Saint-Germain wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Fulham Patrick Roberts. Manchester City pia imeweka nia hiyo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18.

Chanzo: Daily Mail
Jumamosi, Julai 4, 2015 00:00

ARSENAL & LIVERPOOL - PEDRO



Klabu za Arsenal na Liverpool zimezungumza na wakala wa Pedro kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Barcelona. Mchezaji huyo mwenye miaka 27anatarajia kwenda Uingereza, pia Paris Saint-Germain wameonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.

Chanzo: Sport
Jumamosi, Julai 4, 2015 07:58

ATLETICO MADRID - NICO GAITAN & SANTI CAZORLA



Atletico Madrid wanakaribia hatua za mwisho za mazungumzo na klabu ya Benfica kuhusu uwezekano wa kumsajili Nico Gaitan lakini klabu hiyo ya Ureno inahitaji dau la euro milioni 35(£24.9m).

chanzo: Record
Jumamosi, Julai 4, 2015 10:24



Klabu ya Atletico Madrid itarudi kwa kasi kuangalia uwezekano wa kumsajili Santi Cazorla mara baada ya kuondoka kwa Arda Turan. Diego Simeone alimuwania Mhispania huyo zaidi ya miaka miwili lakini klabu ya Arsenal inahitaji ofa kubwa kwa ajili ya mchezaji huyo.

Chanzo: Daily Mail
Jumamosi, Julai 4, 2015 00:23


0 comments:

Post a Comment