TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA...

Saturday, 18 July 2015

DROGBA APEWA OFA MLS:



Klabu ya MLS imempatia ofa ya mkataba nyota mkongwe wa chelsea Didier Drogba, huku Chicago Fire wakiongoza mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea. Hata hivyo kuna upinzani kutoka klabu ya Qatari.

Chanzo: ESPN
Ijumaa,7/17/2015 22:21

ARSENAL WAJIANDAA KUTOA DAU KWA AUBAMEYANG:



Arsenal wanajiandaa kutoa ofa kwa mchezaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Klabu hiyo ya Bundesliga wanataka pauni milioni 31 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.

Chanzo: Reviersport
Ijumaa,7/17/2015 14:02

EVERTON WAHITAJI ADA YA REKODI YA UINGEREZA KWA STONES:



Everton wameitaka klabu ya Chelsea kulipa ada ya rekodi ya Uingereza kama wanahitaji saini wa beki wa klabu hiyo John Stones. Kwa sasa klabu ya Manchester City inashikilia rekodi hiyo ya pauni milioni 31.9 iliyomtolea Eliaquim Mangala.

Chanzo: Daily Mirror
Ijumaa,7/17/2015 22:45

MAN UTD WANAJIPANGA KUMNYAKUA PEDRO:



Manchester United wanajipanga kutoa ofa ya euro milioni 31.5 sawa na pauni milioni 22 kwa ajili ya kumnyaka mchezaji wa Barcelona Pedro na wanamatumaini ya kuipiku klabu ya Chelsea katika harakati za kuiwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Chanzo: Daily Mirror
Ijumaa,7/17/2015 22:35

SOUTHAMPTON WANAKARIBIA KUMPATA VLAAR BAADA YA LAZIO KUJITOA:



Southampton wanakaribia kumnyaka beki wa Aston Villa Ron Vlaar baada ya klabu ya Lazio kujitoa kwenye mbio za kumuwania mchezaji huyo.

Chanzo: Daily Express
Ijumaa,7/17/2015 20:18

BRADY ANAKARIBIA KUJIUNGA NA NORWICH:



Robbie Brady amekataa dili jipya na Hull City huku akiwa anakaribia kujiunga na Norwich kwa ada ya pauni milioni 7.

Chanzo: Daily Mirror
Ijumaa,7/17/2015 20:14

ROMA INAMUWANIA MORENO:



Roma wanajipanga kumuwania mchezaji wa Liverpool Alberto Moreno. Walter Sabatini yupo Uingereza kukamilisha usajili  wa Edin Dzeko na pia anataraji kukutana na maofisa wa Liverpool kuzungumzia ofa ya euro milioni 11.5 (Pauni milioni 8) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Chanzo: Daily Express
Ijumaa,7/17/2015 19:38

MAN UTD WAKATAA KUMUUZA DE GEA BILA RAMOS:



Manchester United wamejiengua wenyewe kutokana na kumpoteza mlinda mlango wao David De Gea ama majira haya ya joto au yajayo, hata hivyo watamuuza kwa kilabu cha Real Madrid kama Sergio Ramos atakuwa sehemu ya makubaliano.

Chanzo: Sky Sports
Ijumaa,7/17/2015 18:09

PORTO WADONDOSHA OFA KWA MITROVIC:



Porto wametoa ofa ya pauni milioni 12.5 katika klabu ya Anderlecht ili kumnyakuwa mshambuliaji wao Aleksander Mitrovic baada ya dau la Newcastle kwa ajili ya mchezaji huyo kukubaliwa. Chelsea pia wameonesha nia kwa mchezaji huyo.

Chanzo: Daily Mirror
Ijumaa,7/17/2015 17:50


0 comments:

Post a Comment