DONDOO ZA USAJILI MAJUU...

Sunday, 19 July 2015

ARSENAL-EDIN DZEKO:



Arsenal wanatazamia kumnyakuwa mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko huku kukiwa na wasiwasi wa bosi wa Arsenal kumtegemea sana Olivier Giroud. Mshambuliaji huyo pia ameivutia klabu ya Roma lakini ana nia ya kuendelea kubaki katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Chanzo: Daily Star
Jumapili,7/19/2015 08:21

MAZUNGUMZO YA DI MARIA NA PSG YAMESIMAMA:



Usajili wa Angel Di Maria kutoka klabu ya Manchester United kwenda PSG umesimama huku kukiwa na ubishani wa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo kati ya vilabu hivyo viwili. Margentina huyo tayari amekwisha kubaliana masharti na mabingwa hao wa Ufaransa, ambao pia wametupia jicho lao kwa Kevin De Bruyne.

Chanzo: L'Equipe
Jumapili,7/19/2015 08:18

MAN UTD BADO INAMNYEMELEA BALE:



Manchester United bado hawajakatisha matamanio yao ya kumnyakuwa mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale, huku Louis van Gaal akipanga kufanya jaribio lingine la kumleta mchezaji huyo wa taifa wa Wales.

Chanzo: Sunday Mirror
Jumamosi,7/19/2015 22:43

STAMBOULI ANAKARIBIA KUJIUNGA NA PSG:



Kiungo wa Tottenham Benjamini Stambouli yupo USA kusaini dili la mkataba wa miaka mitano na klabu ya PSG. Usajili huo utatangazwa rasmi siku ya Jumapili au Jumatatu.

Chanzo: Le Parisien
Jumapili,7/19/2015 11:31

SALAH AKUBALI KUTUA ROMA KWA MKOPO:



Mohamed Salah anajipanga kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo baada ya kukubali kuelekea Serie A. Roma wameipatia klabu ya Fiorentina Matta Destro kama fidia wakati Chelsea wakimuhitaji Alessio Romagnoli kama sehemu ya dili hilo.

Chanzo: Daily Mail
Jumapili,7/19/2015 10:42

ASTON VILLA INAMTAKA CALLUM KAMA MBADALA WA BENTEKE:



Aston Villa wanampango wakumnyakuwa mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson kama mbadala wa Christian Benteke. Mshambuliaji huyo ataigharimu timu hiyo inayonolewa na Tim Sherwood pauni milioni 7.

Chanzo: Daily Express
Jumapili,7/19/2015 09:40

0 comments:

Post a Comment