UNITED YAREJEA KWA MULLER,MADRID YAMSAKA IBRAHIMOVIC,ARSENA YARUDI TENA KWA VARGAS...

Tuesday, 7 July 2015

MANCHESTER UNITED - THOMAS MULLER , MATTEO DARMIAN & RAMOS




Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya euro milioni 82(£58m) kwa ajili ya Thomas Muller. Mh Woodward anatarajia kuzungumza na Karl-Heinz Rummenigge juu ya uwezekano wa kukamilisha dili hilo.

Chanzo: Sport1
Jumanne, Julai 7, 2015 00:09



Mazungumzo baina ya Manchester United na Torino yanaendelea vizuri baada ya Mashetani  Wekundu hao kukaribia kumnyakua Matteo Darmian. Dili hilo la  euro milioni 14 litafanyika haraka, huku Louis van Gaal akiwa tayari kumsajili beki huyo wa kulia.

Chanzo: Gianluca di Marzio
Jumanne, Julai 7, 2015 00:47



Manchester United wameiambia klabu ya Real Madrid kwamba David De Gea hatoweza kwenda Santiago Bernabeu ikiwa Sergio Ramos bado yupo klabuni hapo. Mashetani wekundu hao wamesema watamuachia golikipa huyo endapo watampata beki huyo wa kati.

Chanzo: Manchester Evening News
Jumanne, Julai 7, 2015 00:07

PSG - KEVIN DE BRUYNE



Paris Saint-Germain wameingia kwenye mbio za kumuwania nyota wa Wolfsburg Kevin De Bruyne. PSG walifanya mazungumzo na mchezaji huyo wa ubelgiji mwishoni mwa wiki, lakini klabu ya Manchester City bado wanamatumaini ya kumnyakua mchezaji huyo kwa ada ya euro milioni 70.

Chanzo: Daily Mail
Jumanne, Julai 7, 2015 00:27

BAYERN MUNICH - DI MARIA



Klabu ya Bayern Munich wanajiandaa kutoa ofa kambambe kwa nyota wa Manchester United Angel Di Maria. Bavariani hao watamtoa mchezaji anayesakwa kwa mda mrefu Thomas Muller pamoja na winga Arjen Robben kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo aliyevunja rekodi ya usajili nchini Uingereza.

Chanzo: Daily Mail
Jumanne, Julai 7, 2015 00:47

ARSENAL - EDUARDO VARGAS



Klabu ya Arsenal imerejea kwenye mchakato wa kumnyakua Eduardo Vargas kwa lengo la kuunda uhusiano na mchezaji mwenzake wa Chile Alexis Sanchez.

Chanzo: Corriere dello Sport
Jumanne, Julai 7, 2015 10:32

REAL MADRID - ZLATAN IBRAHIMOVIC



Real Madrid wanafuatilia kwa karibu uhusiano kati ya Zlatan Ibrahimovic na klabu yake ya Paris Saint-Germain. Madrid wapo tayari kutoa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya euro milioni 12(£8.4m) kwa msimu lakini hawawezi kutoa ofa itakayozidi euro milioni 6(£4.2m) kwa mchezaji huyo menye miaka 33.

Chanzo: Sport
Tuesday, July 7, 2015 10:38

TOTTENHAM - TOBY ALDERWEIRELD



Toby Alderweireld amefaulu vipimo vya matibabu katika klabu ya Tottenham ambapo mchezaji huyo anatarajia kujiunga na timu hiyo akitokea Atletico Madrid kwa ada ya £11.5m.

Chanzo: talkSPORT
Jumanne, Julai 7, 2015 14:01

PORTO - IKER CASILLAS



Porto wametoa mkataba wenye ofa ya miaka miwili kwa Iker Casillas, kukiwa na kigezo cha mwaka mmoja mbele, na thamani ya euro milioni 5 kwa msimu. Real Madrid wanampango wa kumuachia mchezaji huyo aondoke bure lakini watakuwa hawajafikia ada ya makazi kwa ajili ya miaka miwili iliyobaki.

Chanzo: Marca
Jumanne, Julai 7, 2015 12:52

LIVERPOOL & TOTTENHAM  -  KEMEN



Liverpool na Tottenham wapo kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Newcastle United mwenye miaka 18 Olivier Kemen

Chanzo: L'Equipe
Jumanne, Julai 7, 2015 11:33

ROMA - EDIN DZEKO



Edin Džeko amekubaliana na klabu ya Roma ili mchezaji huyo ahamie klabuni hapo ambapo atapewa mkataba wa miaka minne na kupokea euro milioni 4.5 kwa msimu lakini klabu hiyo ya Serie A bado hawajakutana na klabu ya Manchester City kujadili uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo kwa ada ya euro milioni 25.

Chanzo: Calciomercato.com
Jumanne, Julai 7, 2015 11:01

INTER - IVAN PERISIC



Klabu ya Inter ipo tayari kumtoa Xherdan Shaqiri kwa ajili ya kupata saini ya Ivan Perisic. Tottenham , Stoke City na Atletico Madrid wote wamekuwa wakimnyatia mchezaji huyo wa kimataifa wa  Uswisi.

Chanzo: Corriere dello Sport
Jumanne, Julai 7, 2015 10:34

VALENCIA - VICTOR VALDES



Golikipa wa Manchester United Victor Valdes ametanabaisha kukataa ofa ya Valencia. Golikipa hiyo mwenye miaka 33 anaimani atakuwa chaguo la kwanza mbele ya Louis van Gaal kama David De Gea ataondoka klabuni hapo.

Chanzo: AS
Jumanne, Julai 7, 2015 11:49

NAPOLI - JOSE CALLEJON



Wakala wa Jose Callejon amepanga kukutana na raisi wa Napoli Aurelio De Laurentiis ili waweze kujadili mustakabali wa mchezaji huyo mwenye miaka 28. Klabu ya Atletico Madrid imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye thamani yake ni kati ya euro milioni 20(£14.2m) na euro milioni 25( £ 17.7m ).

Chanzo: Mediaset
Jumanne, Julai 7, 2015 00:00



0 comments:

Post a Comment