ZA MOTO ULIZOZIKOSA WIKI HII...

Thursday, 9 July 2015

Raheem Sterling

Goal inakuletea dondoo mbali za usajili za nyumbani na kwingineko duniani

Sterling hajaonekana mazoezini Liverpool kwa siku mbili mfululizo

Raheem Sterling ambaye amadhamiria kuihama timu yake msimu huu hajaonekna katika mazoezi ya timu hio kwa kisingizio kwamba anaumwa, Je uhamisho wake umekaribia?

Ramadhani Singano yuko huru kujiunga na timu yoyote

Shirikisho la soka Tanzania limethibitisha kuwa mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ kuwa yupo huru na anaweza kusajiliwa na timu yeyote itakayo muhitaji baada ya klabu yake aliyokuwa akiichezea siku za nyuma Simba kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba

Manchester United kumsajili Darmian, akiri kocha wa Torino

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Italy Matteo Darmian, uhamisho huo ulithibitishwa na kocha mkuu wa Torino Giampiero Ventura aliyekiri kuwa uhamisho huo uko mbioni kukamilika

Tanzania yajitoa All Africa Games

Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema uongozi wa chama hicho umeitaarifu kamati yake juu ya kutoshiriki michuano hiyo itakayoanza September 4-19.

Ukosefu wa fedha umekuwa ni kikwakzo kwa vyama vingi vya michezo nchini Tanzania kushiriki katika michezo mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ya kufuzu michuano mbalimbali ikiwemo hiyo ya Afrika na mengineyo kama vile ya Olimpiki na Jumuiya ya Madola.

Serikali inategemewa kugharamia ushiriki wa wanamichezo kuelekea katika michezo hiyo lakini mpaka sasa haijajulikana ni wanamichezo wangapi watashirki.
Mbali ya baiskeli, Tanzania inategemewa kushiriki katika michezo ya taekwondo, kuogelea, riadha, ngumi na michezo ya watu wenye ulemavu.

Wachezaji wa kimataifa wawasili Azam

Azam ilimaliza nafasi ya pili katka msimu wa ligi uliokwisha na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Shirikisho. Mmoja wachezaji hao ni mlinda lango Mkameruni anayekipiga nchini Congo (DRC ), Nelson Lukong, anayetegemewa kusaili usiku huu.

Mbali na Nelson Lukong leo Alhamisi saa mbili asubuhi kiungo toka nchini England Ryan Burge atawasili na Qatar Air.

Jean Mugiraneze Babtiste toka nchini Rwanda anayekipiga na APR atawasili na Rwanda Air jioni ya leo Alhamisi.

Baada ya mazoezi ya wiki tatu Azam FC inasafiri leo asubuhi kuelekea mjini Tanga, Kaskazini mwa Tanzania kucheza mechi mbili za kirafiki. Itacheza na African sports wana kimanumanu siku ya Jumamosi na Jumapili itakwaana na Coastal Union Mechi zote mbili zitachezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani majira ya jioni.

Timu itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu.

Kocha Wa Taifa Stars awashukuru watanzania

Mkwasa amesema kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo. Uganda (The Canes) ilitoka sare ya 1-1 katika mchezo huo na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-1.

“Kiukweli japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru Mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa.

Murray atinga nusu fainali Wimbledon

Kwa matokeo hayo sasa Murray atavaana na Roger Federer kwenye mchezo utakaopigwa kesho. Federer ametinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kumshinda Gilles Simon raia wa Ufaransa kwa jumla ya set 6-3 7-5 6-2.

Naye bingwa nambari moja ulimwenguni katika mchezo wa tennis Novak Djokovic atamenyana na Richard Gasquet baada ya kumshinda Marin Cilic kwa set 6-4 6-4 6-4.

Young Shepolopolo yawasili Tanzania

Timu hizo zitashuka dimbani siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kikosi cha timu ya Tanzanite chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kimeweka kambi eneo la Mbande na kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Azam Complex kwa takribani wiki ya pili sasa kujiandaa na mchezo huo.

Msemaji wa Shirikisho la soka nchinin Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema hali ya kambi ya Tanzanite ni nzuri wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ya ya hali ya juu, kikubwa Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Msejai wa kuwapa sapoti timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 watakapokuwa wakicheza na wenzao wa Zambia.

She-polopolo wanatarajiwa kuwasili jioni kwa usafiri wa ndege wa shirika la Rwandair ambapo Ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo utachezwa siku ya jumamosi majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi, ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Dunia za Wanawake chini ya miaka 20 (U-20) zitakzofanyika nchini Papua New Guninea mwaka 2016.

Mwamuzi wa mchezo huo ni Batol Mahjob kutoka nchini Sudan, akisaidiwa na washika kibendera Remaz Osaman na Walaa Bilal, mwamuzi wa akiba Khadmallah Elasayed wote kutoka nchini Sudan na Kamisaa wa mchezo ni Flora Roosevelt kutoka nchini Malawi.

0 comments:

Post a Comment