MAN UTD YATIMKIA KWA LUKAKU NA MANDZUKIC,MAN CITY KUMNASA JACK WILSHERE, PAUL POGBA.....

Thursday, 18 June 2015

MAN UTD-LUKAKU,MANDZUKIC;

Romelu Lukaku Everton

Mashetani wa Mnchenster wanafikiria kufanya usajili wa haraka na wakushangaza watu kumnasa mshambuliaji wa Everton Lumelu Lukaku. Huku taharuki hiyo ikitokea mjini Manchester juu ya usajili huo bado wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Athletico de Madrid Mario Mandzukic anaehusishwa pia na miamba ya Italia klabu ya Juventus.



MAN CITY-POGBA,STERLING,WILSHERE;

Manchester City wako mbioni kuzinyaka saini za wachezaji Paul Pogba na Raheem Sterling kutoka Italy na Uingereza. Matajiri hao wanafuatilia kwa karibu wachezaji hao majira haya ya joto.



Baada ya dau la pauni 40 milioni  kukataliwa kumnasa winga wa Liverpool Raheem Sterling. Matajiri hao wa Manchester wahamia kwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Arsenal Jack Wilshere.


R.MADRID-AGUERO;

Real Madrid wanafuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero.


CHELSEA-ROB GREEN;

Chelsea kumuuza Cech Arsenal pengo kuzibwa na Rob Green.Usajili huo wachagizwa na klabu yake ya QPR kushuka daraja.

0 comments:

Post a Comment