MESSI, BALE, CAZORLA....AARON RAMSEY AMTENGENEZA MCHEZAJI WA AINA YAKE...

Friday, 12 June 2015

Messi, Bale, Cazorla... Aaron Ramsey's ultimate footballer

Kiungo wa klabu ya Arsenal Aaron Ramsey amechagua wachezaji kutoka nyumbani na nje ya nyumbani-uchaguzi wa kushangaza na uteuzi wa wachezaji nyota wa timu pinzani-kutengeneza mchezaji wa teknolojia ya kibayoniki (Bionic Footballer).

Nani ni mchezaji mzuri kwa sasa? Tumeshalizungumza sana. Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio bora zaidi kwa sasa-labda kama wewe ni shabiki namba moja wa Javier Mascherano kama Roy Hodgson.

Lakini itakuwaje kama utachanganya na kufananisha? vipi kama Andrea Pirlo angekuwa na guu la kushoto la Messi au Ronaldo angekuwa na muono wa Xavi?

Hivi karibuni tovuti ya Goal imezungumza na Aaron Ramsey kuhusiana na swala hilo. Kiuhalisia alijichagua mwenyewe kama sehemu ya mchezaji wake huyo wa kipekee. Lakini ni nani mwingine alitengeneza daraja? Spoiler: Ronaldo sio mmoja wapo.

Kulikuwa na mishangao michache kwa mchezaji huyo wa Arsenal akitoa heshima kwa chimbuko lake, na pia kwa mashujaa wa Chelsea na wachapakazi wa Liverpool wakihusishwa.

Baada ya kumaliza uchunguzi wa Kibayomekaniki (Biomechanical Tests) kwa ajili ya uwiano mpya, Ramsey alimchagua mchezaji wake huyo wa kibayoniki (Bionic Footballer).

0 comments:

Post a Comment