WACHEZAJI WA JAMAICA WAFURAHIA KIPIGO, WAOMBA KUPIGA PICHA "SELFIE" NA MESSI...

Sunday, 21 June 2015

Messi asked for on-field selfie by Jamaica striker Brown

Kwa sasa mchezaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi atakuwa amezoea kukutana na maombi ya "selfies" kutoka kwa wachezaji na hata mashabiki.

Argentina iliwapiga Jamaica 1-0 Jumamosi ili kujipatia nafasi ya juu ya kundi B katika mashindano ya Copa America, lakini inaonesha wapinzani hao timu ya taifa ya Jamaica waliyafurahia matokeo hayo zaidi kuliko washindi wa mchezo huo Argentina.

Messi, ambaye alikuwa tayari ameombwa jezi yake wakati wa mapumziko, alionekana kutopendezwa na matokeo hayo wakati akitoka nje ya uwanja baada ya mchezo kumalizika, lakini bado alichukua muda wake kukaa na Deshorn Brown baada ya kumpatia jezi yake ya pili ya mchezo huo Jobi McAnuff.



Reggae Boyz , kwa uwazi, walikuwa tu na furaha kuwa karibu mchezaji huyo wa Barcelona.

Brown, ambaye pia alipata "selfie" na mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, alitupia picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram ikiwa na ujumbe, "Sio matokeo tuliyokuwa tukiyatafuta, lakini nimebahatika kukutana na wachezaji bora duniani na ilikuwa ni hisia kubwa kucheza dhidi yake. Namtakia heri Messi pamoja na Argentina katika sehemu ya mashindano iliyobakia."









0 comments:

Post a Comment