PEREZ: KISICHOWEZEKANA KITAWEZEKANA MSIMU UJAO...

Wednesday, 10 June 2015

Perez: Madrid's duty is to make impossible dreams possible

Raisi wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez anasema klabu hiyo itathibitisha kuwa wanaweza kufanya "Haiwezekani" kuwezekana msimu ujao.

Klabu hiyo ya Madrid ilishinda taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya pamoja na Copa del Rey mwaka 2014 lakini hawakuweza kulilinda kombe hilo msimu uliopita pamoja na kukosa kikombe cha ligi na hivyo kunyakuliwa na wapinzani wao klabu ya Barcelona.

Ukosefu wa mataji  katika klabu hiyo umepelekea uamuzi wa klabu hiyo kumtupia virago kocha wao wa zamani Carlo Ancelotti na baadae kumteua Rafa Benitez kama mrithi wake na kumfanya Perez kuwa na matumaini kwamba klabu hiyo itarejea katika makali yake ya awali.

"Tutarudi katika hali yetu ya mapambano muda si mwingi," alisema katika hotuba kutoka VIP box Santiago Benabeu siku ya Jumanne.

"Hiyo ndio njia pekee tumeweza kuonesha ya kuwa ndoto zinaweza kufikiwa, zozote zile, zinazowezekana na zinazoonekana kutowezekana."

"Katika klabu hii unajifunza kutokukata tamaa katika mchezo kama sababu ya kupotea, kupambana hadi sekunde ya mwisho na kurudi tena na nguvu pale tunapopata matokeo tusiyoyahitaji."

Benitez amekuwa kocha wa nne tangu Perez alipochaguliwa kama raisi wa klabu hiyo mnamo mwaka 2009, kipindi ambacho wameonekana wakipata taji moja tu la Ligi.

0 comments:

Post a Comment