TIKETI ZA UEFA EURO 2016 KUANZA KUUZWA...

Wednesday, 10 June 2015



Pamoja na mchezo wa soka kukumbwa na kashfa kubwa, soka la Barani Ulaya limeelekeza macho yake katika mafanikio chanya zaidi.

Ufaransa inaadhimisha mwaka mmoja kuelekea fainali za UEFA Euro 2016 zitakazofanyika katika mji wa mkuu wa Paris.

Rais wa Ufaransa François Hollande amempokea Raisi wa mpira wa miguu wa Barani Ulaya Mfaransa mwenzake Michel Platini katika Elysée Palace kuadhimisha tukio hilo.

Michel Platini amekuwa mtu wa kwanza kupokea tiketi kwa ajili ya mashindano hayo ya #EURO2016 kutoka kwa rais wa Ufaransa François Hollande.

Kwa sasa tiketi hizo kwa ajili ya mashindano hayo ya #EURO2016 zimeanza kuuzwa.

Lakini pamoja na hali nzuri ya mazingira ya mji mkuu wa Paris, kuna wasiwasi kuhusu gharama za mashindano, kifedha na katika suala zima la sifa pia.

Uvumi mkubwa unaoenea kwamba Platini anaweza kuwania nafasi ya uraisi wa FIFA kutokana na raisi wa zamani Sepp Blatter kuachia ngazi hiyo siku za karibuni kutokana na kashfa za rushwa.

0 comments:

Post a Comment