MANCHESTER UTD-BASTIAN SCHWEINSTEIGER:

Manchester United wanakaribia mpango wa pauni milioni 7.5 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger.

Kufuatia uvumi kutoka klabu ya Manchester City kumuhitaji kiungo wa Arsenal Jack wilshere, klabu hiyo yenye makazi yake mjini London imepanga kumpatia kiungo huyo mkataba mpya wenye mshahara mara mbili ya ule aliokuwa anapata mwanzo.
REAL MADRID-DE GEA:

David De Gea amewaambia wachezaji wenzake wa klabu ya Manchester United kwamba anataka kutimka klabuni hapo na kujiunga na miamba wa Hispania klabu ya Real Madrid.
CHELSEA-PETR CECH:

Golikipa wa klabu ya Chelsea ambaye ameomba kutimka klabuni hapo Petr Cech amepewa kiasi cha pauni milioni 4 na bosi wa klabu hiyo Roman Abramovich kama zawadi ya kumuaga.
CHELSEA, MAN CITY-PEPE:

Kufuatia kusimama kwa mazungumzo kati ya klabu ya Real Madrid na mchezaji wake Pepe, klabu za Uingereza, Chelsea na Manchester City, zimeanza kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima ili kutafuta mwanya wa kumsajili beki huyo.
MANCHESTER CITY-RAHEEM STERLING:

Klabu ya Manchester City haijakata tamaa ya kumpata winga wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling baada ya kuongeza dau mpaka kufikia euro milioni 63.
INTER-KONDOGBIA:

Kiungo wa Monaco Geoffrey Kondogbia amekubali kujiunga na miamba wa Italia klabu ya Inter baada ya kuikataa klabu pinzani ya AC Milan. Mchezaji huyo ataigharimu klabu hiyo ada ya euro milioni 35 na atahudhuria vipimo vya afya kesho Jumatatu.








0 comments:
Post a Comment