HALI IMEZIDI KUWA MBAYA KWA MARIO BALOTELLI

Saturday, 1 August 2015



Liverpool walikamilisha usajili wenye gharama ya pauni milioni 16 kumnyaka nyota wa Italia kutoka katika kilabu cha AC Milan Mario Balotelli ambaye ameshindwa kuwika katika klabu ya Liverpool na kwa sasa hali imekuwa mbaya kwa mchezaji huyo aliyeambiwa abaki akifanya mazoezi peke yake baada ya kilabu hicho kuelekea Finland kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya HJK.

Haya yote yamezidi kumkumba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 baada ya kutuma ujumbe kumsifia mchezaji Raheem Sterling aliyetimka kilabuni hapo kuelekea Manchester City na kufanikiwa kutupia katika mchezo wake wa kwanza katika klabu yake hiyo mpya.

Lakini muonekano huu unadhihirisha kuwa maisha ya Mario katika kilabu hicho yamefikia ukingoni baada tu ya msimu mmoja tangu ajiunge kutokea AC Milan ambapo amefanikiwa kutupia magoli 4 tu katika michezo 28 aliyotokea, huku goli moja kati ya magoli hayo likiwa ni la Ligi Kuu.



Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers alisema wiki iliyopita huko Kuala Lampur ambapo walishiriki ziara yao ya maandalizi ya msimu kuwa amemuachia Mario mwenyewe kuamua maisha yake ya baadae.

Bologna ni klabu ya Serie A inayomuwania Balotelli, ambaye ana miaka miwili iliyosalia katika mkataba wake ambao analipwa pauni 90,000 kwa wiki, lakini Liverpool hawajapokea ofa rasmi yoyote kwa ajili ya mshambuliaji huyo mtukutu.

Imeripotiwa kuwa Balotelli amekuwa akifanya mazoezi kila siku, pamoja na beki wa kushoto wa Hispania Jose Enrique na Fabio Borini ambao wanaonekana kutokuwa na nafasi katika kikosi cha Brendan.

0 comments:

Post a Comment