WENGER: SANCHEZ NI BORA KULIKO HUYO HAZARD

Saturday, 1 August 2015



Kocha Arsene Wenger amesema staa wa Chelsea, Eden Hazard hajafikia kiwango cha kuanza kumwingiza kwenye kundi la mafundi kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Wenger alisema hata nyota wake kwenye kikosi cha Arsenal, Alexis Sanchez anaweza kumfunika Hazard katika msimu huu.
Akizungumza na ESPN, kocha huyo Mfaransa alisema: “Labda ukiniambia ni maoni tu ya mtu hapo sawa. Kama kwa kulinganisha namba tu, naweza kusema Messi na Ronaldo wanafunga hadi mabao 50 na kuwa peke yao. Hakuna mpinzani. Sitaki kuzungumzia hilo. Kila mtu nafikiri anadhani mchezaji wake ni bora kitu ambacho kinaeleweka tu. Nikimtazama Sanchez kwa kitu ambacho amekifanya katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu England ni cha kipekee.
“Nina imani hatarudia tu, bali ataongeza zaidi. Hazard anaweza kubadili mechi na utaweza tu kumweka daraja hilo kama atafanya hivyo mara kwa mara.”



Arsenal na Chelsea watamenyana siku ya kesho katika mchezo wa ngao ya hisani huku wadau wa soka duniani wakiamini huenda Wenger akapata ushindi wake wa kwanza mbele ya vijana wa Jose baada ya kumnyakuwa mlinda mlango mahiri Petr Cech kutoka katika kilabu hicho pinzani msimu huu.

0 comments:

Post a Comment